Trump awasili Saudi Arabia

Rais Donald Trump akikaribishwa kwa bashasha kubwa na ukoo wa kifalme wa Saudi Arabia jana , wakati akiweka kando, japokuwa kwa muda tu , utata mkubwa unaoukumba utawala wake mjini Washington. Rais Trump akilakiwa mjini Riyadh Trump amewazawadia wenyeji wake mpango wa mauzo ya bilioni 110 wa silaha wenye lengo la kuimarisha usalama wa Saudi Arabia pamoja na makubaliano kadhaa ya kibishara. "Hii ni siku muhimu sana, uwekezaji mkubwa katika Marekani ," Trump alisema wakati wa mkutano na mwanamfalme Mohammed bin Nayef. Rais Trump (Kushoto) akisalimiana na mfalme wa Saudi Arabia Salman bin Abdulaziz(kulia) Ziara katika mji mkuu wa Saudi Arabia iliku...